Full-Width Version (true/false)


K.SHEIN KUONGOZA KIKAO CHA NEC TAIFA Z’BAR MAY 27, 2018.

 

 
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuongoza kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.
 
Kikao kitafanyika siku ya Jumapili  May 27, 2018 katika Ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui kuanzia majira ya saa 4:00 asubuhi.
 
Pamoja na mambo mengine kikao kitapokea na kujadili taarifa mbali mbali kutoka katika Idara na vitengo vya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar.
 
Kikao hicho kitakuwa cha kawaida kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 1977 Toleo la 2017, Ibara ya 108 (2).
 
Aidha Chama Cha Mapinduzi kinaeleza kuwa kikao hicho ni miongoni mwa vikao vyake vya Uongozi vya Kitaifa vinavyofanyika kwa mujibu wa Kanuni na miongozo ya CCM.

No comments

Powered by Blogger.