Full-Width Version (true/false)


KUKABILIANA NA MMOMONYOKO WA MAADILI, NGUO FUPI ZAPIGWA MARUFUKU CHUONI.

Ili kukabiliana na mmomonyoko wa maadili miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Zambia, Chuo Kikuu cha Zambia kimetangaza kupiga marufuku nguo fupi kwa wananfunzi wa kike wawapo maktaba katika chuo hicho.

Marufuku hiyo imetangazwa kupitia mbao za matangazo chuoni hapo, ikiwemo mbao za matangazo kwenye maktaba ya chuo, ambapo sababu za marufuku hiyo zimetajwa kuwa ni usumbufu amabo wamekuwa wakiupata wanafunzi wa kiume wawapo maktaba hapo.

Marufuku hiyo imesema kuwa wanafunzi wa kiume wamekuwa wakipoteza umakini wa kile wanachokisoma wakiwa maktaba, na hivyo kujikuta wanapoteza muda wao mwingi kutazama miili ya wanafunzi wa kike ambayo kwa kiasi kikubwa huwa imeachwa wazi.

Maarufuku hiyo imelalamikiwa na wanafunzi wa kike wakidai kuwa haiwatendei haki, huku wakisema sababu ya kuwa wanafunzi wa kiume wamekuwa wakipoteza umakini haina mashiko maana ni uzembe wao wenyewe, huku wakihoji kama huenda maktaba kusoma kwanini wapoteze muda kuwaangalia wasichana ambao nao huwa wanajisomea.

Kwa upande wao wanafunzi wa kiume wamepokea kwa furaha marufuku hiyo, huku wakisema itawasaidia kuweka akili yao kwenye kusoma wawapo maktaba, tofauti na hapo awali ambapo walipoteza muda wao mwingi kuwashangaa wanafunzi wa kike.

Suala la mavazi mafupi imekuwa changamoto kubwa kwenye vyuo vikuu kote duniani, ambapo wanafunzi wa kike wamekuwa wakilalamikiwa kuvaa mavazi mafupi kiasi cha kuwatia vishawishini wanafunzi wa kiume, na baadhi ya walimu wakiume vyuoni.

No comments

Powered by Blogger.