Full-Width Version (true/false)


Kumbe kisa Diamond: Harmonize aeleza sababu ya kutompa mkono Alikiba
Msanii wa muziki Bongo, Harmonize amefunguka sababu ya kutompa mkono Alikiba pindi walipokutana katika msiba wa Agness Masogange.

Muimbaji huyo anayefanya vizuri na ngoma ‘Kwa Ngwaru’ ameiambia The Playlist ya Times FM kuwa mambo yote yanayozungumzwa si ya kweli, bali walisalimiana ila si kwa kushikana mikono.

“Unajua asilimia kubwa ya watu wanaozungumza hawakuwa pole, unajua unapomzungumzia Alikiba ni mtu ambaye amefanya muziki wetu upate heshima kwa namna moja au nyingine kama msanii namuheshimu siwezi nikakutana na mtu halafu nisimsalimie, sio kweli,” amesema.

“Kilichofanyika ni kwamba Diamond kamsalimia kwa mkono, wamesamiliana kwa mkono. Mimi nimekuja nimezunguka nikaona kwa kuwa Diamond kamsalimia kwa mkono, kamgeuzia kiganja mimi nikamsalimia kwa sauti tu, tukakaa pale tukaendelea,” amesisitiza Harmonize.

Diamond na Alikiba walikutana April 22, 2018 katika viwanja vya Leaders Dar es Salaam ambapo palikuwa panafanyika misa ya kuuaga mwili wa aliyekuwa video vixen Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ ambaye alifariki April 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.