Full-Width Version (true/false)


Kumetangazwa visa vipya vya ugonjwa wa Ebola vimeibuka DR Congo


Kumetangazwa visa vipya vya ugonjwa wa Ebola kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Kuna visa viwili vilivyothibitishwa na watu 17 waliofariki, wizara ya afya imesema.

Wataalam wa maradhi ya Ebola kutoka wizara ya afya nchini Congo leo Jumatano wanatarajiwa kuambatana na wale wa shirika la afya duniani WHO kwenda jimboni Equateur baada ya kuthibitishwa kuwepo kwa visa hivyo.

Kisa kilichotokea katika mji wa Bikoro kinajiri zaidi ya mwaka baada ya mlipuko wa ugonjwa huo kusababisha vifo vya watu wanne nchini humo, Mnamo 2014 zaidi ya watu 11,000 waliuawa nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia.

Tangazo la kuzuka kwa visa hivyo vipya limetolewa baada ya matokeo ya uchunguzi wa maabara kuthibitisha visa viwili vya Ebola kati ya sampuli za wagonjwa watano waliokuwa wanahsukiwa, Shirika la afya duniani (WHO) limesema.

"Lengo letu kuu ni kuushirikisha mji wa Bikoro na serikali,"Msemaji wa WHO Peter Salam alisema katika taarifa yake.

"Kushirikiana na washirika na kukabiliana na visa mapema katika namna iliyoratibiwaitakuwa ni muhimu katika kuudhibiti ugonjwa huuu hatari."

Shirika hilo la afya duniani linasema limetoa $ milioni 1 kutoka fuko la dharura na limetuma zaidi ya wataalamu 50 kufanya kazi na maafisa nchini Congo, Hii ni mara ya tisa kunazuka ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Virusi vya ugonjwa huo viligunduliwa kwa mara ya kwanza katika nchi hiyo iliyokuwa ikijulikana kama Zaire, mnamo 1976 na jina lake linatokana na mto Ebola.

Inadhaniwa kwamba Ebola husambazwa katika maeneo ya mbali kupitia popo na husambazwa miongoni mwa binaadamu kutokana na kula nyama za mwituni.

No comments

Powered by Blogger.