Full-Width Version (true/false)


''Kuna Waziri nikimuona nakimbia'' - Musukuma

Mbunge wa Geita Vijijini Mh. Joseph Musukuma amesema baadhi ya Wizara ni kichefuchefu na kuna Waziri hata akifumba macho akifumbua akamuona anakimbia kutokana na anavyofanya kazi zake katika Wizara anayoongoza ndio maana baadhi wamepata taabu kupitisha Bajeti zao Bungeni. 
Akiongea leo Mei 23, kwenye kipindi cha KIKAANGONI kupitia Ukurasa wetu wa Facebook , Musukuma amewataja baadhi ya Mawaziri wanaozitendea haki Wizara zao kuwa ni Waziri William Lukuvi wa Ardhi na Ummy Mwalimu wa Afya.

''Unajua sio kila Wizara unachangia tu zingine zimekamilika hata Mawaziri wake waliposimama kusoma Bajeti zao ili zipitishwe hakuna aliyepinga, lakini kuna Waziri hata ukinifumba macho nikifumbua tu nikamuona nakimbia'', amesema.

Musukuma amesema baadhi ya Mawaziri wamekuwa wakifanya kazi kwa mihemuko ndio maana wao kama wabunge wanajitahidi kuwashauri wanapokuwa wameenda tofauti.

Aidha ameeleza kuwa kitendo cha Wabunge kushauri vitu kadhaa Bungeni hawamaanishi lazima wasipitishe bajei ila wanachofanya ni kushauri kisha kupitisha ili serikali ikafanyie kazi ushauri wao.

No comments

Powered by Blogger.