Full-Width Version (true/false)


Kundi la IS ladai kuhusika shambulizi nchini Libya

Kundi la itikadi kali linalojiita Dola la Kiislamu (IS) limedai kuhusika na shambulizi la jana Jumatano katika ofisi za makao makuu ya tume ya uchaguzi nchini Libya liilowaua kiasi cha watu 12 na kuwajeruhi wengine saba.

Wafanyakazi watatu wa tume ya uchaguzi na maafisa wanne wa vikosi vya usalama nchini Libya ni miongoni mwa waliouawa.

Dulu kutoka nchini humo zinasema mtu mmoja alijitoa muhanga akiwa ndani ya ofisi za tume hiyo ya uchaguzi inayojiandaa kwa ajili ya uchaguzi baadaye mwaka huu.

No comments

Powered by Blogger.