Full-Width Version (true/false)


Lema awataka wanaume wanyooshe mkonoMbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema amefunguka na kuwataka wanaume wenzake kujitathmini na kujibadilisha baadhi ya tabia zao ndani ya familia ili mwisho wa siku waweze kuwalea watoto wao wa kike katika misingi iliyokuwa bora. 
Lema amebainisha hayo asubuhi ya leo kupitia ukurasa wake maalum wa twitter baada ya kuwepo wimbi la kubwa la wababa wenye tabia chafu na mbaya huku wao wenyewe wakiwakatalia watoto wa kike wasiolewe na wanaume wenye tabia kama zao.

"Katika mahubiri Mchungaji aliuliza 'ni baba gani hapa angependa mtoto wake aolewe na baba mwenye tabia kama zake anyooshe mkono!. Sikumbuki kama niliona mkono. katika siku hii ya 'Mother's day' njia pekee ya kuithamini siku hii ni mwanaume kuwa teyari kunyoosha mkono kwa swali kama hili", amesema Lema.

Godbless Lema ametoa ujumbe huo kama sehemu ya kuwakumbusha wanaume umuhimu wa kubadilika na kuacha vile ambavyo wao hawapendi watoto wao wa kike wafanyiwe.

No comments

Powered by Blogger.