Full-Width Version (true/false)


Lewandowski aomba kuondoka Beyern Munich


Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Poland, Robert Lewandowski ameomba kuondoka katika Klabu yake ya FC Bayern Munich ya nchini Ujerumani.


Lewandowski ambaye bado ana mkataba na mabingwa hao wa Bundesliga hadi mwaka 2021, amemkodi Wakala Pini Zahavi amsaidie kufanya mazuyngumzo ili Klabu hiyo imuachie. Zahavi ni wakala aliye nyuma ya mafanikio ya Neymar na dili lake la kwenda PSG.


Hivi karibuni baada ya kumalizika kwa Bundesliga, Lewandowski alionekana akiwa na wakala wa Mardid. Lewandowski, mwenye umri wa miaka 29, amefunga mabao 151 katika mechi 195 tangu alipojiunga na FC Bayern akitokea Dortmund kwa uhamisho huru mwaka 2014.


Kwa misimu kadhaa sasa, Lewandowski amekuwa akihusishwa na kujiunga na Real Madrid, na sasa wakala wake Pini Zahavi amethibitisha kwamba ni kweli mteja wake anataka kuondoka Allianz Arena. Chelsea, PSG ni vilabu vingine ambavyo vinahusishwa na uhitaji wa saini ya Robert.

No comments

Powered by Blogger.