Full-Width Version (true/false)


Licha ya kufungwa 4-2,Liverpool yatinga fainali UEFA

Klabu ya Liverpool imefanikiwa kutinga hatua ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa  Ulaya UEFA licha ya kufungwa mabao 4 kwa 2 na AS Roma ya nchini Italia.

Liverpool FC wanasonga mbele kwa faida ya magoli waliyofunga katika mchezo wa awali walioshinda mabao 5 kwa 2 hiyo kuwa na hazina ya magoli 7 kwa 6 ya AS Roma.


Katika mchezo uliomalizika usiku wa kuamkia leo May 3,2018 magoli ya Liverpool yamewekwa kimiani na Sadio Mane 9' na Georgio Wijnaldum 25' huku yale ya AS Roma yakifungwa na Milner(aliyejifunga), Edin Džeko 52' na Radja Nainggolan 86' na 90+2'.


Liverpool FC sasa itakwaana na Real Madrid katika mchezo wa Fainali unaotarajiwa kupigwa katika dimba la Olympic National Sports Complex huko Jijini Kiev nchini Ukraine.


Mchezo huo utapigwa tarehe 26 mwezi May,2018

No comments

Powered by Blogger.