Full-Width Version (true/false)


LICHA YA KUWA MAJERUHI, NEYMAR AITWA KIKOSINI BRAZIL


Nyota wa PSG, Neymar Jr, ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia inayotaraji kuanza mwezi Juni huko Russia.

Mshambuliaji huyo ambaye hali yake bado haijaimarika kiafya vizuri, ameunganishwa na wachezaji wengine 22 wa kikosi ambao tayari wameshaitwa.

Neymar aliumia mwezi Machi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya katika mchezo dhidi ya Real Madrid kwenye hatua ya 16 bora kwa kufungwa jumla ya mabao 5-1.

Wachezaji ambao wameitwa kwenye kikosi hicho ni;-

Makipa: Alisson (Roma), Ederson (Manchester City), Cassio (Corinthians).
Mabeki: Danilo (Manchester City), Fagner (Corinthians), Marcelo (Real Madrid), Filipe Luis (Atletico Madrid), Thiago Silva, Marquinhos (both PSG), Miranda (Inter Milan), Pedro Geromel (Gremio).
Viungo: Casemiro (Real Madrid), Fernandinho (Manchester City), Paulinho (Barcelona), Fred (Shakhtar Donetsk), Renato Augusto (Beijing Guoan), Philippe Coutinho (Barcelona), Willian (Chelsea), Douglas Costa (Juventus).
Washambuliaji: Neymar (PSG), Taison (Shakhtar Donetsk), Gabriel Jesus (Manchester City), Roberto Firmino (Liverpool).

No comments

Powered by Blogger.