Lipuli yafafanua kwa nini waligoma Salamba kwenda Yanga lakini wamekubali aende Simba

Uongozi
wa klabu ya Lipuli umelitolea ufafanuzi suala linaloezwa kuwa
iliwabania makusudi Yanga kuwaazimisha aliyekuwa mchezaji wao Adam
Salamba na badala yake amesajiliwa Simba.
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ramadhani Mahano, amezungumza na kueleza kuwa kuna vitu ambavyo Yanga waliwaeleza lakini walishindwa kwenda nao sawa.
Mahano amesema Yanga waliwapa taarifa kuwa mchezaji huyo asingeweza kutumika ndani ya timu tatu katika msimu mmoja kwani kanuni za soka haziruhusu.
Kiongozi huyo amefafanua akisema kuwa kwa mujibu wa TFF, CAF na FIFA hawaruhusu mchezaji mmoja kuzitumika klabu zaidi ya mbili ndani ya msimu mmoja hivyo ilikuwa ngumu kuwapatia.
Tayari mchezaji huyo ameshamwaga wino na wekundu wa Msimbazi ikiwa ni baada ya msimu kumalizika kwa kusaini mkataba wa miaka mwili na katika msimu ujao atakuwa sehemu ya kikosi hicho.
No comments