Full-Width Version (true/false)


LIPULI YAGOMA KUWAPATIA YANGA SALAMBA, YAWASHAURI WATAFUTE MCHEZAJI MWINGINE

Uongozi wa klabu ya Lipuli FC umewajibu Yanga kuhusiana na barua yao iliyotumwa ikihitaji ombi la kupatia Mshambuliaji wao, Adam Salamba ili akaisaidie timu yao kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Ikumbukwe Yanga walituma barua kwenda Lipuli wakiomba wapatiwe mchezaji Salamba ili awape nguvu katika mashindano ya kimataifa kutokana na baadhi ya wachezaji wao haswa katika safu ya ushambuliaji kukumbwa na majeraha.

Kwa mujibu wa barua kutoka uongozi wa Lipuli, imeeleza kuwa baada ya Kamati ya Utendaji wa klabu hiyo kukutana na kulijadili suala hilo, umefikia maamuzi ya kutoweza kuwapatia Yanga mchezaji wao.

Aidha barua imeeleza kuwa kwa mujibu wa kanuni za CAF. FIFA NA TFF haziruhusu mchezaji mmoja kuchezea klabu zaidi ya mbili kwa msimu mmoja, hivyo itakuwa ni vigumu kuwapatia.

Aidha, Lipuli imewashauri Yanga kutafuta mchezaji mwingine badala ya Salamba kwa manufaa ya klabu yao.


No comments

Powered by Blogger.