Full-Width Version (true/false)


LIPULI YATHIBITISHA KUPOKEA BARUA YA YANGA WAKIMWOMBA SALAMBA, UONGOZI YANGA WATOA TAMKOUongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa tayari walishatuma barua ya kumuomba mchezaji nyota wa Lipuli, Adam Salamba ili aisaidia timu hiyo katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga leo itakuwa inafanya mazoezi yake ya mwisho kuelekea mechi na Rayon Sports itakayopigwa Uwanja wa Taifa kesho Jumatano majira ya saa moja usiku.
Kwa mujibu wa Dismas Ten ambaye ni Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano katika klabu ya Yanga, amesema wanachokisubiri hivi sasa ni majibu kutoka kwa Lipuli ambao wamethibitisha kupokea barua hiyo.
Hata hivyo uongozi wa Lipuli umekuwa ukisita kutoa jibu rasmi kuhusiana na kuwaazima Yanga mchezaji huyo kwa muda.
Ukiachana na Lipuli kupokea barua hiyo, dalili zinaonesha kuna asilimia chache ya kuweza kumruhusu kutokana na uongozi wa klabu hiyo kuleta ngumu kutoa majibu ya moja kwa moja kuhusiana Salamba kama ataenda Yanga.

No comments

Powered by Blogger.