Full-Width Version (true/false)


LIVERPOOL YAANZA KUMYATIA KIPA HUYU BRAZIL KUCHUKUA NAFASI YA KARIUS


Tetesi kutoka Barani Ulaya zinaeleza kuwa Liverpool ipo kwenye mchakato wa kumtafuta mbadala wa mlinda mlango wao, Loris Karius.


Taarifa zilizoripotiwa na mitandao mbalimbali barani humo zinasema kuwa Liverpool inamnyatia kwa karibu kipa Mbrazili, Allison Becker anayeichezea Roma pamoja na Msolavania Jan Oblack anayekipiga Atletico de Madrid ya Spain.


Hatua hiyo imekuja mara baada ya kipa tegemo wa Liverpool, Rolis Karius kushindwa kufanya vizuri katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid uliopigwa juzi Jumamosi.


Karius aliweza kuruhusu mabao matatu huku mawili yakileta utata juu ya kiwango chake na kupelekea Liverpool waanze kumsaka mbadala wake mapema.

No comments

Powered by Blogger.