Mabosi wa kampuni iliyomtapeli Mzee Majuto mamilioni wawekwa rumande

Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema
kuwa kuna Kampuni iko Mwanza iliingia Mkataba na King Majuto na Mkataba
huo ulikuwa ni wakumlipa Milioni 24 wakatoa check, check hiyo ikawa
haina Pesa, Hivyo serikali imewachukulia hatua wahusika.
“Naomba niwaeleze wananchi Nimeunda jopo la wanasheria na tumeshaanza
kikao cha kwanza sasa hivi kazi yetu kubwa kwasababu tumeshaanza na
suala la Mzee Majuto ni kuangalia kazi zote akizokwisha zifanya na
tunawaandikia barua wote waliohusika watupe mikataba wanayoijua wao
tutakaa nao tuanza kuchambua mkataba mmoja baada mwingine na
tutawataarifu itakavyo fuatia,” amesema Dkt. Mwakyembe
“Kuna kampuni moja ya Mwanza waliingia Mkataba na King Majuto na
Mkataba huo ulikuwa ni wakumlipa Milioni 24 wakatoa check, check hiyo
ikawa haina Pesa tunashukuru uongozi wa Mwanza kwa kushirikiana nao
wahusika wako ndani na tutaendelea kuchukua hatua kali kwa watu ambao
wanadhani wanaweza kutumia jasho la wenzao kujinufaisha wenyewe,”
alisisitiza.
No comments