Full-Width Version (true/false)


“Madrid walitaka kunisajili”- Iniesta
Mchezaji wa zamani wa klabu ya FC Barcelona Andres Iniesta, amedai kwamba alikuwa akipokea maombi ya mara kwa mara kutoka kwa wapinzani wao wakubwa timu ya Real Madrid, ikimtaka ajiunge na timu hiyo iliyopo katika  Jiji la Madrid nchini Hispania.  

Kwa mujibu wa gazeti la michezo la 'The Sun' limesema kwamba Iniesta amesema hayo leo Mei 28, 2018 na kuongeza kuwa timu ya Real Madrid ilikuwa ikijaribu kumshawishi ingawa mchezaji huyo hakuwakaribisha katika meza ya  mazungumzo.

“Kuna muda Madrid walionekana kuvutiwa na mimi, kulikuwa hakuna majadiliano ukiachilia mbali ukweli ni kwamba sikutaka kuwa katika timu ile” amesema Iniesta. 

Andres Iniesta angekuwa ni mchezaji wa nne kutoka Barcelona  kujiunga moja  kwa moja na wapinzani wao Real Madrid baada ya wachezaji wa zamani wa timu hiyo Luis Figo, Michael Laudrup na Bernd Schuster.

Mei 24, 2018 mchezaji Andres Iniesta mwenye umri wa miaka 34 alijiunga na klabu ya Vissel Kobe ya ligi kuu nchini Japan, akitokea timu ya FC Barcelona aliyoichezea kwa takribani miaka 22.
 

No comments

Powered by Blogger.