Full-Width Version (true/false)


Mahudhurio hafifu ya wanafunzi wa kike yapatiwa ufumbuzi
Katika kuonesha kuwa wanaunga mkono na kuthamini suala la elimu kwa watoto wa kike, Watumishi wanawake wa Manispaa ya Ilala  wameanzisha kampeni waliyoipa jina la 'Binti makini mwamvuli wangu stara' yenye lengo la kujenga vyoo kwenye shule zilizopo kwenye manispaa hiyo.

Kupitia tafiti mbalimbali zinazofanyika kuhusiana na sababu zinazochangia mahudhurio hafifu ya watoto wa kike mashuleni hususani wale wa darasa la saba zinaeleza kuwa vyoo hafifu na visivyofaa kwa watoto wa kike kipindi cha hedhi ndiyo sababu kubwa ya mahudhurio hayo.

Hivyo kwa kutambua changamoto hiyo inayowakabili watoto wa kike, Watumishi hao wamesema wameanzisha kampeni ya kujenga vyoo maalumu ambavyo vitawawezesha kushiriki kikamilifu masomo yao badala ya kubakia nyumbani wakati wa hedhi hali inayoathiri mtiririko wa maudhui ya yale yanayofundishwa shuleni.

" Uzinduzi wa kampeni hii unatarajiwa kufanyika Mei 11, mwaka huu katika ukumbi wa Lamada na mgeni rasmi atakua Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, tunashukuru namna ambavyo watumishi wa manispaa walivyojitoa kuhakikisha kuwa tunafanikisha azma yetu hii ya kuwasaidia watoto hawa ambao ni watoto wetu, wadogo zetu pia.

" Kampeni ya ujenzi wa choo kwa ajili ya mtoto wa kike itaanzia kwenye shule 120 za msingi zilizopo kwenye manispaa ya Ilala na kuendelea katika shule za sekondari, tunaamini lengo letu la kuondoa zile siku nne ambazo takwimu zinasema watoto hawa ndio wanakua wanazipoteza ndani ya mwezi mmoja sasa zitaondoka kwa kuwa changamoto imetatulika," amesema Mratibu wa Kampeni hiyo Tabu Shaibu.

Choo kitakachojengwa kitakuwa na matundu 10, maji ya kutosha, masinki ya kunawia mikono, kabati la kuhifadhi taulo za kik, kioo na sehemu ya kuchomea taka. Gharama za ujenzi zinakadiriwa kufikia sh 20,000,000.

No comments

Powered by Blogger.