Full-Width Version (true/false)


Majaliwa awaonya Wakuu wa Mikoa


 


Waziri Mkuu, amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanasimamia vizuri suala la usafi wa mazingira katika maeneo yao la sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. 
Amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa kutatua tatizo la usafi wa mazingira pamoja na miundombinu hususani katika masoko hali ya kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zinakusanya fedha nyingi bila kuboresha maeneo na kukithiri kwa  uchafu.

Mheshimiwa Spika Kupitia Bunge lako tukufu, nawaagiza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi pamoja na Maafisa Afya wasimamie zoezi la usafi na kuboresha miundombinu yote na utawapima kupitia zoezi hili,” amesema.

Waziri Mkuu amesema suala la usafi limekuwa likifanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi baada ya kuasisiwa na Rais Dkt. John Magufuli, hivyo ametumia fursa hiyo kuwaagiza watendaji hao wahakikishe maeneo yao yanakuwa safi na miundombinu inayoweza kutumika wakati wote.

No comments

Powered by Blogger.