Full-Width Version (true/false)


Makonda apewa siku 30Mamlaka ya Mapato nchini Tanzania (TRA), imempa siku 30 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwenda kulipia ushuru kontena zake 20 na kuzichukua kuanzia Jumatatu Mei 21, 2018 na endapo atashindwa kufanya hivyo basi mamlaka hiyo itazipiga mnada. 
Kontena hizo za Makonda ambazo zimesubiri utaratibu wa kuzitoa TRA kwa zaidi ya siku 90 zinazokubalika kwa mujibu wa sheria za kodi, zimesheheni samani za ndani na ofisini.

Akizungumza na waandishi wa habari Mei 16, 2018 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA Richard Kayombo, amesema kwa kawaida bidhaa zote zinapoagizwa na kufika bandarini zinatakiwa kuondolewa ndani ya siku 90.

Aidha, Kayombo amesema inapotokea muda huo ukapita bila wahusika kuondoa mizigo yao, hujulishwa na mamlaka hiyo kwa kupewa notisi ya siku 30 ili waondoe.

Kwa mujibu wa tangazo la TRA lililotoka kwenye vyombo vya habari Jumatatu, Mamlaka hiyo imetoa notisi ya siku 30 kwa wateja nane akiwamo "Paul Makonda" ambao mizigo yao imekaa bandarini zaidi ya muda unaotakiwa.

"Tumetoa tangazo hili ili kontena ambazo ziko bandarini ambazo zimepitiliza siku 90 wahusika waende kuziondoa na wasipotekeleza ndani ya muda tuliowapa tutazipiga mnada kwa mujibu wa sheria. Siwezi kusema kama wameshindwa kulipa kodi au la lakini hata ikitokea bidhaa ambazo zina msamaha wa kodi zimekaa zaidi ya siku zilizowekwa na wamiliki wakapewa notisi bila kutekeleza, muda wa notisi ukiisha bidhaa husika hupigwa mnada na kwenye hili hatuangalii bidhaa zimetoka wapi, ni msaada au sio msaada",amesema Kayombo.

Kwa upande mwingine, Kayombo amesema bidhaa zilizoagizwa zikapitiliza siku za kukaa bandarini kwa mujibu wa taratibu huwa wanatangaza bila ya kuangalia zimeagizwa na nani, kuna nini ndani yake, zimelipiwa ama hazijalipiwa na kama hazijaondolewa bandarini basi wanatangaza kama walivyofanya

No comments

Powered by Blogger.