Full-Width Version (true/false)


Man City yaungana na Real Madrid na BarcelonaBao la Gabriel Jesus dakika za mwisho kwenye mchezo kati ya Mabingwa wa EPL Manchester City na Southampton jana jioni, liliifanya timu hiyo kufikisha alama 100 msimu huu na kuifikia rekodi ya klabu za Real Madrid, Barcelona na Juventus. 
Manchester City ambayo inafundishwa na Mhispania Pep Guardiola, imeweka rekod hiyo kwa mara ya kwanza kwenye ligi kuu ya soka nchini England baada ya ushindi huo wa jana ambapo mshambuliaji wa Kibrazil Gabriel Jesus alifunga bao pekee dakika ya 90.

Kabla ya hapo tayari Man City ilikuwa imeshatwaa ubingwa wa ligi hiyo baada ya kufikisha alama ambazo zisingefikiwa na timu iliyoshika nafasi ya pili Manchester United hivyo mchezo wa jana ulikuwa ni wa kutafuta rekodi na kulinda heshima tu.

Kwa upande mwingine timu ambazo zimewahi kufikisha alama 100 katika ligi tano bora duniani ni Real Madrid ilipofanya hivyo msimu wa 2011/12, Barcelona msimu wa 2012/13 na Juventus msimu wa 2013/14.

Man City imetwaa ubingwa kwa tofauti ya alama 19, ikiwa na pointi 100 huku nafasi ya pili ikishikwa na Manchester United wakiwa na 81. Mfungaji na mchezaji bora wa ligi hiyo msimu huu ni Mohamed Salah ambaye ni raia wa Misiri.

No comments

Powered by Blogger.