Full-Width Version (true/false)


MANARA AAHIDI KUWAUMIZA YANGA KWA STAILI HII


Ofisa wa Habari katika klabu ya Simba, Haji Manara, ameahidi kutoa yake ya moyoni endapo Simba itaweza kuutangaza ubingwa Jumamosi ya wiki hii.

Simba itakuwa inahitaji pointi moja pekee ili kufikisha kuutangaza ubingwa wa Ligi Kuu Bara endapo itaweza kwenda sare dhidi ya Singida United kwenye mchezo wa ligi utakaopigwa Mei 12 2018.

Manara ameeleza kufanya tambo za kila aina kwa watani zake wa jadi Yanga ikiwa ni baada ya Simba kuukosa ubingwa wa ligi kwa zaidi ya miaka takribani mitano.

Kiongozi huyo mbwembwe za aina yake, amesema kwa sasa anahifadhi maneno na hataki kusema lolote akisubiri Jumamosi baada ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Namfua ndiyo atakuwa ana la kusema.

Mpaka sasa Simba walio vinara wa ligi wana alama 65 huku Yanga wakiwa na pointi 48 pamoja na michezo mitatu mkononi.

Wakati huo Singida United wametamba kulipiza kisasi na kuvunja rekodi ya Simba ambayo haijapoteza mchezo wowote mpaka sasa, hii ni baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-0 kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza.

No comments

Powered by Blogger.