Full-Width Version (true/false)


Manara atoa ahadi ya kulitikisa BungeMkuu wa Habari na Mawasiliano wa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) Simba SC, Haji Manara amefunguka na kutoa ahadi ya kuwa katika msimu ujao wa ligi 2018/19 timu yake itafanya makubwa mpaka kupelekea Bunge kutengua baadhi ya kanuni zake. 
Manara ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa kijamii mara baada ya uongozi wa Simba kiujumla kuhudhuria shughuli za Bunge kwa siku ya leo kutokana na mualiko waliopewa na Spika wa Bunge Job Ndugai katika siku za hivi karibuni.

"Mabingwa wa nchi ndani ya mjengo, asanteni Wabunge wote kwa heshima kubwa mliyotupa leo. Nawaahidi mwakani kwa tutakayoyafanya mtatengua kanuni ili tuingie ndani na kuwa sehemu ya Bunge", amesema Manara.

Simba sasa imefikisha alama 68 kileleni katika michezo 28 ikiwa imebakiza mechi mbili kuweza kumaliza msimu huu.

No comments

Powered by Blogger.