Full-Width Version (true/false)


Manara awapa ujanja mashabiki wa Simba

Ukiachana na Simba kukabidhiwa ubingwa wa VPL msimu huu, watani zao Yanga wamekuwa wakiwasakama kutokana na kupoteza mchezo wao wa kwanza msimu huu dhidi ya Kagera Sugar siku ambayo walikabidhiwa kombe.

Yanga wanaitania Simba kwa kufungwa mbele ya Rais Magufuli ambaye alikuwa mgeni rasmi siku hiyo na kuwakabidhi Simba kombe.

Haji Manara amehoji mashabiki wa Yanga wanaoicheka Simba kupoteza mechi moja huku wakiwa mabingwa wakati wao wameshapoteza mechi tano.

“Watani zetu wanaacha kuzungumzia kufungwa kwao wanazungimzia Simba kushindwa kumaliza ligi bila kupoteza mchezo.”

“Wewe umeshafungwa mechi tano kwenye ligi halafu unashangilia mtu ambaye kafungwa mechi moja kwenye ligi ni vitu ambavyo vinachekesha.”

“Mashabiki wetu wala isiwakere, wao ni mabingwa wa nchi na hilo ndio lilikuwa lengo kuu haya mengine yalikuja njiani baada ya kuona kwamba inawezekana kumaliza ligi bila kupoteza mechi.”

“Tungeshinda hata 10-0 halafu ubingwa tusichukue hata huyo Rais asingekuja.”

No comments

Powered by Blogger.