Full-Width Version (true/false)


Manara aweka nia kuisaidia Yanga kwa sharti hili

Afisa Habari wa timu ya Mabingwa Tanzania Bara, Haji Manara ameweka nia yake ya kutaka kuandaliwa mechi kati ya Simba  na watani zao wa jadi Yanga ili waweze kuwasaidia kiuchumi kwa kuwapatia mapato yatakayokusanywa katika mchezo huo. 
Manara ameyasema hayo ikiwa ni katika kuendeleza utani wake kwa klabu hiyo ambayo imeshindwa kutetea ubingwa wake katika msimu huu huku ikidhaniwa kwamba ni kutokana na hali ngumu ya kiuchumi inayopitia klabu hiyo.

Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram leo ameweka picha ya gari la klabu ya Yanga ambalo likionekana limepata hitilafu  na kusema kwamba kati mechi hiyo sharti wanalotoa kwa watani zao ni kuwapa shikamoo Simba.

"Nina jaribu kuongea na wenzangu klabuni tuone namna ya kucheza mechi ya kirafiki na hawa jamaa ili wachukue mapato yote ya uwanjani kuwanusuru na swaumu yao..hata sijui kama bima imelipiwa hii gari" Manara.


Ameongeza "Sharti la hiyo mechi Gongowazi wote watuamkie..Shikamoo Simba.

No comments

Powered by Blogger.