Full-Width Version (true/false)


MANARA: SIMBA NDIYO KLABU GHALI KULIKO ZOTE AFRIKA MASHARIKI NA KATIIkipewa asilimia 98 ya kuutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano katika klabu ya Simba, Haji Manara, amesema Simba ndiyo klabu ghali Afrika Mashariki na Kati.

Manara ameeleza hayo kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda jana kwa kusema kuwa hakuna dalili za kuukwepa ubingwa, na hii inatokana na namna ilvyojiwekeza kwa kuwa na wachezaji wengi wazuri msimu huu.

Akizungumza kupitia Radio One, kwenye kipindi cha Michezo, Manara ametamba kwa kueleza ubingwa kuelekea Simba kutokana na ughali wa kikosi hicho kuliko timu zote za Afrika Mashariki na Kati.

Manara amefunguka kuwa Simba ina thamani ya Bilioni 1.3 huku akiamini kwa namna kikosi hicho kilivyo msimu huu hakuna atakayeweza kuwazuia wasiuchuku ubingwa.

No comments

Powered by Blogger.