Full-Width Version (true/false)


MARCEL KAHEZA ATHIBITISHA RASMI KUSAINI SIMBAMshambuliaji aliyekuwa anichezea Majimaji FC, Marcel Kaheza, amethibisha kusaini mkataba wa awali na klabu ya Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu nchini msimu huu.


Kaheza ambaye ambaye amehitimisha safari ya kuichezea Majimaji FC iliyoshuka daraja rasmi leo baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Simba, atakuwa na kikosi cha wekundu hao wa Kariakoo katika msimu ujao wa ligi.


Mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kuichezea Simba akikuzwa kutoka kikosi B, anakuwa anarejea kwa mara ya pili Msimbazi baada ya kupachika mabao 14 kwenye ligi akiwa na Majimaji msimu huu.


Mbali na Kaheza, taarifa zimeeleza pia kuwa Simba imeshanyaka saini ya Mshambuliaji wa Lipuli FC, Sadam Salamba.


Baada ya Kaheza aliyekuwa wa kwanza kusaini na Simba, Salamba anakuwa mchezaji wa pili kujiunga na mabingwa hao mara 19 katika Ligi Kuu Vodacom.

No comments

Powered by Blogger.