Full-Width Version (true/false)


Marekani yaomba Burundi ‘kuisamehe’ VOA


Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Utangazaji wa Mashirika ya Serikali ya Marekani (BBG) ambayo inasimamia shirika la habari la Sauti ya Amerika (VOA), John Lansing amemuomba Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza kutengua uamuzi wake wa kufungia matangazo ya VOA kurushwa nchini humo.

Wiki iliyopita Burundi ilifungia matangazo ya mashirika ya VOA na BBC kwa kipindi cha miezi sita kwa madai ya kukiuka maadili ya uandishi wa habari.

Lansing ameeleza kuwa bodi hiyo itaendelea kuwaunga mkono raia wa Burundi kwa kutoa matangazo ya kuaminika na yasiyopotosha.

No comments

Powered by Blogger.