Full-Width Version (true/false)


Mashabiki wa Liverpool wanaowasili Roma kushuhudia UEFA waonywa

Mashabiki wa klabu ya Liverpool wanao wasili Roma nchini Italia kushuhudia mchezo wa nusu fainali ya pili dhidi ya mwenyeji timu ya AS Roma wameonywa na jeshi la polisi kutozurura hovyo pasipo sababu wakati wa mchezo huo.Maelfu ya mashabiki wa Liverpool wamewasili kwenye jiji la Roma huku hali ya ulinzi ikionekana kuimarika kila kona kuelekea ngwe ya pili ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kwanza kupigwa nchini Uingereza na Liverpool kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 5 – 2 dhidi ya AS Roma.Kuzuia kwa mashabiki hao kunakuja kufuatia hofu ya kuvunjika kwa hali ya usalama huku hofu kubwa ikiwa ni kufanyiwa vitendo vya vurugu baadhi ya wafuasi wa Liverpool kutoka kwa wapinzani wao Roma.

No comments

Powered by Blogger.