Full-Width Version (true/false)


Mashabiki wa Simba Songea wakesha

 

Kilichowatokea Simba ndani ya mji wa Songea ni hatari tupu unaambiwa, mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo wamewapokea kwa shangwe jambo lililowashtua viongozi na wachezaji wa timu hiyo.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara ambao kwa msimu huu kwao ni wa 19, wametua Songea jana Jumamosi na mapokezi yalikuwa ya nguvu, lakini si hapo tu huko njiani walipopita hadi wanaingia ndani ya mji huo ilikuwa ni shida.
Meneja wa Simba, Robert Richard amesema: "Songea ni shida yaani, tumepokewa  vizuri na kwa shangwe kubwa, watu walikuwa wengi sana kuanzia barabarani tulipopita hadi tunafika."
Songea inaaminika kuwa na mashabiki pamoja na wapenzi wengi wa Simba ambao huenda ni Zaidi ya mikoa mingi Tanzania wamekuwa wakiiunga mkono timu hiyo mara kwa mara.
Simba ipo Songea kwa ajili ya mchezo wao wa ligi kuu kukamilisha ratiba ya mechi zao za msimu huu wa ligi kuu dhidi ya wenyeji wao Majimaji.


No comments

Powered by Blogger.