Full-Width Version (true/false)


Mbao FC yachezesha mgonjwa isishuke darajaIkiwa ligi kuu soka Tanzania Bara inaelekea ukingoni, klabu nya Mbao FC ya Mwanza imezichanga vizuri alama zake katika vita ya kukwepa kushuka daraja na kuziacha timu tatu kwenye hatari ya kuikosa ligi kuu msimu ujao. 
Mbao FC ambayo jana ililazimika kumchezesha nahodha wake Yusuph Ndikumana, ambaye anasumbuliwa na Malaria ili tu kusaka ushindi dhidi ya Stand United, lengo hilo lilitimia na kuibuka kidedea kwa bao 1-0 ugenini. bao hilo limewaondoa Mabo FC kwenye hatari ya kushuka.

Timu hiyo amabyo ipo kwenye msimu wake wa pili tangu ipande daraja, imefikisha alama 30 na kwenda katika nafasi ya 13, ikiziacha timu za Majimaji FC yenye alama 24 katika nafasi ya 14, Ndanda alama 23 nafasi ya 15, Njombe Mji alama 22 nafasi ya 16.

Msimu huu zitashuka timu mbili zitakazomaliza katika nafasi za 15 na 16, ili kuzipisha timu 6 zitakazopanda msimu ujao na kukamilisha timu 20 kwaajili ya msimu wa ligi kuu 2018/19.
Bao pekee lililowaokoa Mbao FC, llifungwa na nahodha Yusuph Ndikumana ambaye pamoja na Malaria alijikiza kuweza kuitetea timu yake isishuke daraja. Hata hivyo nahodha huyo aliomba kutoka dakika ya 59 baada ya kuona hali yake hairuhusu kuendelea na mchezo.

No comments

Powered by Blogger.