Full-Width Version (true/false)


MBAO FC YAJIWEKEA MAZINGIRA MZAURI KUSALIA LIGI KUU KWA KUIFUNGA NDANDA FC CCM KIRUMBA LEOBao pekee la Vincent Philipo lillilofungwa katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza limeiwezesha Mbao FC kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa jijini Mwanza.
Matokeo hayo yameizidi kuiweka Ndanda kwenye mazingira mabaya ya kuteremka daraja huku yakiipa faida Mbao ya kujitengenezea nafasi nzuri kuendelea kusalia kwenye ligi.
Msimamo wa Ligi Kuu unaonesha Mbao imejiongezea alama kwa kufikisha idadi ya pointi 27 na kupanda kwa nafasi moja kutoka ya 15 mpaka 14.
Wakati huo wapinzani wa Mbao FC, Ndanda, wamezidi kusalia chini wakiwa na alama zao 23 katika nafasi ya 15.

No comments

Powered by Blogger.