Full-Width Version (true/false)


Mbunge aionya serikali, Spika aunga mkonoMbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Singida (CCM), Martha Mlata ameitaka Serikali kuachana kabisa na suala la chapa ya mifugo kwa kuwa inaumiza mnyama bila sababu za msingi. 
Katika mchango wake kwa Wizara ya Mifugo, Mlata amesema mambo yanayofanywa na Wizara hayaonyeshi kabisa kama wizara hiyo inaongozwa na wasomi .

Mbunge huyo amepinga suala la operesheni akisema haliko sahihi kwani kuna watu wanaonewa bila sababu za msingi na kwa namna moja linawanufaisha upande wa serikali tu.

Kuna msomi gani huko wizarani ambaye anaruhusu kuchoma vyuma vya moto na kuwachoma wanyama wetu bila sababu za msingi, hivi hakuna namna nyingine ya kuweka alama hizo?” amehoji Mlata.

Hata hivyo Hoja hiyo imeungwa mkono na Spika wa Bunge Job Ndugai, ambaye amesema Wizara imeshindwa kufanya mambo kisomi hata kufananisha wazee wa zamani ambao waliweka alama mifugo yao na ilitambulika vizuri ingawa hawakuwa wamesoma lakini walithamini mifugo yao na kuwa na huruma.

No comments

Powered by Blogger.