Full-Width Version (true/false)


Mbunge aitaka serikali kuruhusu uvunaji wa TemboMbunge wa Jimbo la Kavuu (CCM), Dkt. Pudesiana Kikwembe, ameitaka Serikali kuruhusu wananchi wanaoishi karibu na hifadhi za wanyama, kuuwa tembo kwaajili  ya kitoweo ikiwa kama njia ya kupunguza idadi ya wanyama hao wanaovamia makazi na mashamba. 
Mbunge Kikwembe amesema hayo leo Mei 21, 2018 Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kuchangia hoja mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara  Maliasili na Utalii katika mwaka wa fedha 2018/2019.

“Tembo tunasema wapo hatarini kupotea, lakini kila siku tunalaalmika tembo wanavamia mashamba, vijiji vyote nilivyovitaja hakuna mahindi, tembo wamevamia, mimi nasema (Tembo) wapo wengi ndiyo maana wanaenda kule, kwanini tusifanye utaratibu wa kuwavuna na hiyo nyama ikaliwa na wananchi ili tuwapunguze” amesema Dkt. Kikwembe.

Mbunge huyo ameongeza kuwa serikali haiwezi kuzuia wanyama hao wasiingie katika mashamba kutokana na idadi kubwa ya tembo ambao wanazidi kuzaliana na hivyo njia pekee ni kuandaa utaratibu kwa kuwapa wananchi kibari cha kuvuna tembo hao

Bunge kwasasa linajadili Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii katika mwaka wa fedha 2018/2019 na waziri wake Dkt Hamis Kigwangalla ameomba wabunge kuizinisha jumla ya shilingi bilioni 115.7 za Wizara hiyo, ambapo bilioni 85.8 ni kwaajili ya matumizi ya kawaida na bilioni 29.9 ni fedha za miradi ya maendeleo.

No comments

Powered by Blogger.