Full-Width Version (true/false)


Mbunge ataka Kiswahili kitumike kuanzia Chekechea mpaka chuo KikuuMbunge wa Kuteuliwa, Abdallah Bulembo(CCM) ameitaka serikali kutoona aibu na kufanya maamuzi magumu kuruhusu Kiswahili kifundishwe kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu.

Bulembo ameyasema hayo Bungeni Mjini Dodoma wakati akichangia Bajeti wa Wizara ya Elimu na Teknolojia ambapo amesema kuwa serikali biashara ya kizungu itakutana nayo huko Ulaya.

“Nianze kwa huu muundo wa shule ya msingi na Sekondari hawa walioanzia 20, 15 tangu sera imetungwa wataenda mpaka darasa la sita lakini hapo nyuma 20,14 tunawatu wa darasa la sita na la saba je serikali yangu imejiandaa kupokea hawa wanafunzi watakao maliza darasa la kwa wakati mmoja? amehoji.

Bulembo aliongeza, “Suala la elimu awamu ya tano kwenye elimu bure ni suala linaloenda kumuangalia mtoto wa maskini na elimu hii sio kwa wale mliozaliwa mnasoma tu wale watoto wa wavuvi, wakulima wasisome hapana, tunaposema elimu bure huyu mama anayepika kitumbua mtoto wake asome ndiyo dhamira ya serikali iliyopo.”

“Mimi nafikiri ifikie mahali serikali ifanye maamuzi na maamuzi yenyewe yawe magumu tu kama tunaanza chekechea mpaka form five mpaka six ni Kiswahili iwe Kiswahili basi kwasababu mtoto anapojifunza anaangalia ni Lugha gani anajifunza kutoka kwao, hakuna mzazi mwenye mtoto ambaye amejifungua akaanza kizungu labda nyie mjini ndio mnafanya hivyo, lakini vijijini ni Kiswahili, sasa tunakikwepaje kiswahili kwenda kujifunza Lugha za watu wengine? Ndiyo Lugha yetu kwahiyo Kiswahili kina nafasi kubwa sana ulimwenguni watu wanaotaka kujua Kiswahili ni wengi wanaotaka kujifunza kutoka kwetu ni wengi tunakiogopa cha nini me nasema serikali biashara ya kizungu mtakutana nayo huko Ulaya, embu tuamue kiswahili kutoa Chekechea mpaka chuo Kikuu dhambi ni ipi? kwanini tuna kwepa chetu fanyeni maamuzi tu kuna watu wanasema kweli Kiswahili ni kigumu lakini kwasababu hatukufundishwa tunaongea tu,” alisisitiza.

No comments

Powered by Blogger.