Mbunge Lema aichambua kazi ya Bunge
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA) amesema kazi ya Bunge ni kuisimamia serikai.
Lema, leo Mei 12 amedai kuwa Tanzania kazi ya Bunge ni kusimamiwa na serikali huku akiwata wananchi kuelewa hivyo.
“Kazi ya Bunge ni kuisimamia Serikali,Tanzania kazi ya Bunge ni
kusimamiwa na Serikali,hivi ndivyo wananchi wanapaswa kuelewa,Bunge
ambalo haliwezi kusimamia haki ya Mbunge aliyepigwa risasi kupata haki
yake,bunge hilo halitaweza kujua shida zenu za maji hata kama mnakufa na
kiu,” ameandika Lema kupitia mtandao wake wa Kijamii.

No comments