Full-Width Version (true/false)


Mbwana Samatta atua Mecca kufanya UmrahMbali na soka lakini mchezaji wa Taifa Stars na Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta ni mtu wa ibada.

Mchezaji huyo baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya Ubelgiji ametua mjini Mecca nchini Saudia Arabia kwa ajili ya kufanya ibada ya Umrah.
Mbwana Samatta (kushoto) akiwa na mchezaji mwenzake wa Genk, Omar Colley

Kwenye ziara hiyo, Samatta ameambatana na mchezaji mwenzake wa Genk, Omar Colley ambaye ni raia wa nchini Gambia.

Samatta anatarajiwa kurejea hapa nchini muda sio mrefu kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa hisani wa kuchangia elimu kati yake na timu ya Alikiba kwenye mchezo ambao unatarajiwa kuchezwa Juni 9, mwaka huu.

No comments

Powered by Blogger.