Full-Width Version (true/false)


Mchekeshaji Idris Sultan ameamua kumtania Ben Pol kuhusu shati lake alilovaa siku ya May 14, 2018 katika uzinduzi wa ngoma yake mpya Clouds FM  na kuomba watu wamchangie fedha za kununua nguo mpya  kutokana na shati hilo kuchanika.

Idris ameandika utani huo kupitia ukurasa wake wa instagram na kusema kuwa tusimkumbuke mtu kwenye mazuri tu anapokufa bali katika uhai wake akipata shida tumsaidie.

“Wasanii huwa tunasubiri mpaka kuwe na msiba ndio tuungane kumsaidia mwenzetu kwani dalili kama hizi za kukosa nguo hatuzioni ? Kwanini tusimsaidie Ben angali hai ?”

“Kaka mpaka ananyoa kipara kubana sabuni tunakaa tu hatujiongezi ila tunajua kujifanya Dah RIP alikua noma sana Samboira aliambiwa ajichunge sijui kama kajichunga, shida yule demu ali touch phone yake naye nimemaindi.”


No comments

Powered by Blogger.