Full-Width Version (true/false)


Mchezaji Azam kuelekea Afrika Kusini kwaajili ya Matibabu


Wakati Azam FC ikiwa inatarajia kuanza safari leo kuelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya kibarua dhidi ya Stand United, mchezaji Yakubu Mohammed anatarajia kusafiri leo kuelekea Afrika Kusini.

Mohammed anaenda Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu kufuatia kuumia na kupelekea kukosekana Uwanjani kwa muda mrefu.

Afisa Habari wa Azam, Jaffer Idd Maganga, amesema mchezaji huyo ataondoka leo nchini kupata matibabu ili aweze kurejea kikosini kujiunga na wenzake.

Azam Fc itakuwa inakipiga na Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara Mei 6 2018 kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

No comments

Powered by Blogger.