Full-Width Version (true/false)


Mechi ya Mtibwa na Singida FA kiingilio buku tu

 

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza viingilio vya mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya Mtibwa Sugar na Singida United utakaopigwa siku ya Jumamosi jijini Arusha. 

Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo, amevitaja viingilio hivyo kuwa cha chini ni shilingi elfu moja (Sh. 1000), mzunguko A na B ni shilingi elfu mbili (2000) wakati VIP ni shilingi elfu kumi (Sh.10000). 

Ndimbo amesema, maandalizi ya mchezo huo kila kitu kinakwenda vizuri na kwamba suala la usalama na mambo mengine yako vizuri. 

Mtibwa na Singida zinacheza mchezo huo ambao mshindi kati yao ataiwakilisha nchini kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

No comments

Powered by Blogger.