Full-Width Version (true/false)


Mechi ya Yanga yapelekwa usiku 
Mabingwa wa soka nchini na wawakilishi pekee wa kimataifa klabu ya Yanga, wanatarajia kucheza mchezo wa pili wa hatua ya makundi dhidi ya Rayon Spots, mchezo ambao utapigwa saa 1:00 usiku. 
Mchezo huo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Yanga na Rayon Sports ya nchini Rwanda utachezwa Mei 16 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Shirikisho la soka nchini (TFF) mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Angola na tayari shirikisho la soka Africa (CAF), limeshaitumia Yanga na TFF majina ya waamuzi na kamisaa wa mchezo.

Yanga ilicheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya U.S.M Alger wikiendi iliyopita nchini Algeria na kukubali kipigo cha mabao 4-0. Matokeo ambayo yameifanya kushika mkia katika kundi D.

Kundi hilo linaongozwa na U.S.M Alger yenye alama 3, ikifutiwa na Gor Mahia ya Kenya yenye alama 1 sawa na Rayon Sports yenye alama 1. Baada ya mechi ya Rayon Sports Yanga itacheza na Gor Mahia.

No comments

Powered by Blogger.