Full-Width Version (true/false)


Messi awatumia mabeki salamu wajipange Kombe la Dunia


Buenos Aires, Argentina. Nahodha wa Argentina Lionel Messi ametuma salamu kwa mabeki wa timu pinzani katika fainali za Kombe la Dunia, baada ya kufunga mabao matatu ‘hat-trick’.
Mshambuliaji huyo alifunga mabao hayo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Haiti ambao Argentina ilishinda 4-0.
Pia mchezaji nguli wa timu hiyo Mascherano alipewa tuzo kwa kufikisha idadi ya mechi 143 za kimataifa sawa na nyota wa zamani, Javier Zanetti.
Mshambuliaji wa Manchester City, Sergio ‘Kun’ Aguero alifunga bao moja katika mchezo huo wa maandalizi ya Kombe la Dunia.
Mascherano, anayepewa nafasi ya kuvunja rekodi ya Zanetti, alikwenda uwanjani akiwa ameongozana na mwanaye wakati wa kupewa tuzo hiyo.
Beki huyo wa zamani wa Liverpool, amewahi kucheza na Messi katika kikosi cha Barcelona.
Timu hiyo inayonolewa na kocha Jorge Sampaoli inatarajiwa kuvaana na Israel wiki ijayo katika mchezo mwingine wa kirafiki kabla ya kuanza kampeni kuwania ubingwa wa dunia Juni 16. Argentina itaanza kwa kumenyana na Iceland kabla ya kuzivaa Croatia na Nigeria katika fainali hizo. 

No comments

Powered by Blogger.