Mh. Mabula awafunda watumishi wa wizara ya ardhi
Watumishi wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wameaswa
kuijiepusha na vitendo vya rushwa ili kuendelea kuongeza tija.
Akizungumza wakati akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa
Wizara hiyo leo, mjini Dodoma Naibu Waziri wa Wizara hiyo,Dkt. Anjelina
Mabula amesema kuwa watumishi wa Wizara hiyo lazima watambue kuwa rushwa
ni adui mkubwa wa haki.
“Hatuwezi kutoa haki kama tunapokea rushwa hivyo naagiza kila
mtumishi awe mlinzi wa mwenzake, ukimwona mtumishi mwenzako anajihusisha
na vitendo hivyo ni vyema akachukua hatua ya kutoa taarifa kwa mkuu
wako wa kazi ili hatua stahiki zichukuliwe,” alisisitiza Mabula.
Aidha Mabula alisema kuwa ni vyema watumishi wote wakajitathmini ili
kuona ni wapi tunahitaji kujipanga upya ili kukidhi matarajio ya
watanzania katika huduma zinazotolewa kwa wananchi.
Hata hivyo, Mabula alitoa wito kwa watumishi wote kuendelea kufanya
kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za Usimamizi wa sekta ya
Ardhi nchini.
No comments