Full-Width Version (true/false)


Mke wa Trump afanyiwa upasuaji wa figoMke wa Rais wa  Marekani Melania Trump amefanyiwa upasuaji wa figo.
Ofisi yake imesema kuwa madaktari walifanya upasuaji huo kwenye hospitali ya Walter Reed National Military Medical Center na hakukuwa na matatizo yoyote kwa mujibu wa msemaji wake.

Rais Trump aliandika katika 'Twitter' kuwa alikuwa njiani kwenda kumtembelea hospitalini.


Wiki iliyopita Bi Trump alizindua mpango kwa jina "Be Best" wenye lengo la kuwafunza watoto kuhusu masuala ya kijamii, afya kuhusu hisia na kimwili.
 

No comments

Powered by Blogger.