Full-Width Version (true/false)


Mkuu wa mkoa wa Ruvuma akagua vituo vya afya Madaba

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe Christina Mndeme amekagua ujenzi wa kituo cha Afya cha Mtyangimbole Kata ya Mtyangimbole Halmashauri ya Wilaya ya Madaba 
 
 Mhe Mndeme ameelezwa kuwa kukamilika kwa kituo hicho ni hatua muhimu sana ya utoaji wa Huduma za Afya kwa wananchi wa eneo hili kwani huduma Bora za Afya hazikuwepo kwa miaka mingi na kuwafanya wananchi wa kata ya Mtyangimbole na kata jirani kusafiri umbali mrefu kwenda hadi Songea kupata huduma ya Afya. 

Aidha Mhe Mndeme ,amesisitiza Halmashauri  hiyo kukamilisha haraka ujenzi wa kituo hicho ili wananchi waanze kupata huduma Kwa sababu Serikali Kuu imeisha toa fedha yote kwa ajili ya ujenzi huo.

No comments

Powered by Blogger.