Full-Width Version (true/false)


MKWASA ATAJA SABABU ILIYOPELEKEA YANGA KWENDA SULUHU NA RAYON

 

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, ametoa sababu za kikosi chao kwenda sare ya kutokufungana dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Mkwasa ameeleza kuwa kugawanyika kwa wachezaji wa Yanga kwa ajili ya mechi za ligi huku wengine wakisalia Dar es Salaam ni sababu mojawapo iliyoleteleza mechi hiyo kwenda sare.
Katibu huyo amesema kuwa kuwagawa wachezaji hao imeleta uchovu fulani haswa kwa wale waliokuwa nje ya Dar es Salaam hivyo kushindwa kuonesha kiwango kizuri dhidi ya Rayon.
Vilevile ameeleza kuwa endapo wachezaji wote wangekuwa pamoja na wenzao waliokuwa wamesalia Dar es Salaam wangeweza kuonesha kitu tofauti Uwanjani na ingewezekana matokeo yangekuwa tofauti.
Yanga ilishindwa kutamba katika mchezo huo baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 ambapo sasa katika msimamo wa kundi D ipo nafasi ya 4 ikiwa na alama moja pekee.

No comments

Powered by Blogger.