Full-Width Version (true/false)


Mo Dewji aweka wazi sababu za kupenda soka kuliko michezo mingineMfanyabiashara maarufu nchini Tanzania na Shabiki mkubwa wa Simba, Mohammed Dewji (Mo Dewji) amefunguka sababu za kuupenda zaidi mchezo wa soka kuliko michezo mingine.Kupitia mtandao wa Instagram, Dewji amesema sababu za kuupnd mchezo huo ni kutokana na kuwa unganisha watu bila kujali dini, rangi ya ngozi, kabila, utajiri, umri au jinsia.“Unajua kwanini napenda mpira wa miguu? Kwa sababu soka linaunganisha watu wote! Soka halibagui dini, rangi ya ngozi, kabila, utajiri, umri au jinsia. Kila mmoja anaweza kufurahia soka, na hili ni moja ya mambo machache duniani ambayo yanawafanya watu kuwa wamoja,” ameandika Dewji kwenye picha hiyo hapo juu aliyoiweka kwenye mtandao huo.

No comments

Powered by Blogger.