Full-Width Version (true/false)


Mo Dewji kuibeba Simba rasmi Mei 20

Uongozi wa klabu ya Simba unatarajia kufanya Mkutano wa Mabadiliko ya katiba utakaofanyika siku ya Jumapili ya Mei 20, 2018.

Kwa mujibu wa afisa habari wa klabu ya Simba kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram ameandika kuwa wanakwenda kukamilisha mchakato rasmi tarehe 20 mwezi huu kwakuwa mpira ni pesa kauli inayoashiria kukamilika kwa mabadiliko hayo ya katiba kutampa wepesi mshindi wa dhabuni ya timu hiyo, Mohammed Dewji kukabidhiwa majukumu rasmi.
Tunakwenda kukamilisha mchakato rasmi tarehe 20 mwezi huu..Mpira ni pesa sio porojo za kutegemea kuuza majarida..na uzuri wake MO anakuja kuwekeza pesa..ni pesa tu…..tunahesabu siku tubadilishwe hadhi…ila tunaomba kombe letu mapema kwa hiyari yenu….hahahahaha naambiwa foreigners kaenda mmoja tu..wengine hadi wapewe mishahara
Swap kulia uone taarifa ya mkutano wetu…. Acha nicheke kigongowazi
Uongozi wa klabu ya Simba umetoa taarifa kuwa unatarajia kufanya mkutano wake wa dharura Mei 20 mwaka huu
Uongozi wa klabu ya Simba unatarajia kufanyika Mkutano wa Mabadiliko ya katiba utakaofanyika siku ya Jumapili ya Mei 20, 2018.
Mkutano huo muhimu unatarajia kufanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere uliopo maeneo ya Ocean Road hapa jijini Dar es Salaam majira ya saa 3 asubuhi.
Uongozi wa klabu ya Simba unatarajia kuwatumia ajenda na nyaraka wanachama wake siku chache zijazo ikiwa nikwa mujibu wa katiba yao ibara ya 22 kifungu namba nne inavyowaelekeza.

No comments

Powered by Blogger.