Full-Width Version (true/false)


MOHAMMED DEWJI ARIDHIA ASILIMIA 49 SIMBA BILA KINYONGO
Bilionea na Mwanachama wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji 'Mo'. ameridhia kuwekeza hisa zake katika klabu ya Simba zilizo na asilimia 49.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Simba SC, Haji Manara, amesema kuwa tajiri huyo kijana amekubali kufanya hivyo baada ya serikali kuamua ni lazima mwekezaji apate kiwango hicho cha asilimia na wanachama wakipatiwa 51.
Hapo awali Dewji alihitaji kuwekeza hisa za asilimia 51 huku zitakazosalia zitakuwa za wanachama lakini baadaye serikali ikaingilia kati na kupinga suala hilo na kuamua ziwe 49 pekee kwa mwekezaji.
Kuafuati serikali kuleta maamuzi hayo, kulikuwa taarifa zilizokuwa zinaripoti kuwa Dewji amejitoa kufuatia serikali kubadilisha kiwango cha mwekezaji kuwa na 49% badala ya 51% lakini Manara ameeleza kuwa zilikuwa hazina ukweli wowote.
Simba itakuwa na mkutano mkuu wa dharura na wanachama wake utakaohusika na mabadiliko ya katiba Mei 20 Jumapili ya wiki hii.

No comments

Powered by Blogger.