Full-Width Version (true/false)


Monalisa na Chemical walivyofunga wiki na vazi la ungo ‘Lupahero’Wiki hii imekua na matukio mengi, lakini katika mitindo ni lile inalowahusu wasanii wa kike , Monalisa kutoka Bongo Movie na Chemical mwanamziki wa Rap, wakiwa wameonekana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii wakiwa wamevalia mavazi ya nyungo ambazo zimetobolewa.


Mtindo huo wa uvaaji umeanzishwa na au kubuniwa na mbunifu wa maleba/mavazi Jocktan Makeke maarufu kama Makeke International.

Makeke ameiambia Bongo5 kwamba mtindo huo unaitwa LUPAHERO , jina ambalo limetokana na kuunganishwa maana ya ungo kwa jina la kinyakyusa na kihehe.Hata hivyo Lupahero imeshika kasi hivi karibuni kama mtindo wa mavazi ya kitamaduni yanayotumia ungo kubeba dhima ya ushujaa pale yanapovaliwa na kufanya mvaaji kutambulika kama shujaa.Msanii wa filamu Monalisa na msanii wa muziki Chemical hivi karibuni wamedhihirisha kuwa moja ya wanawake mashujaa baada ya kuvaa mavazi ya LUPAHERO ambayo ni alama ya ushujaa kwa mwafrika.

No comments

Powered by Blogger.