Full-Width Version (true/false)


MOROGORO:Mwalimu awapa adhabu ya kuzibua vyoo bila kuvaa 'gloves' Wanafunzi

MOROGORO: Mwalimu awapa adhabu ya kuzibua vyoo bila kuvaa 'gloves' Wanafunzi wa Kike wa Shule ya Sekondari SUA
Mwalimu huyo alichukua hatua hiyo baada ya kubaini vyoo vya shule hiyo vimeziba kutokana na Wanafunzi hao kutupa taulo za kike katika matundu ya vyoo hivyo

Wanafunzi hao wamelalamikia kitendo hicho kwakuwa si cha kiungwana, kimewaathiri kisaikolojia pia ni hatari kwa afya zao

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Manispaa ya Morogoro, amesema kuwa alifika shuleni hapo na kumuhoji Mwalimu anayetuhumiwa kutenda kitendo hicho pamoja na uongozi wa shule

Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kumwambia Mwalimu huyo aandike barua ya kuomba kuhama kwa gharama zake mwenyewe

No comments

Powered by Blogger.